Pata taarifa kuu
Mali-Uasi

Rais wa Mali Amani Toumani Toure asema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

Rais wa Mali Amadou Toumani Toure amesisitiza nchi yake kufanya uchaguzi mkuu wa uraisi mwezi wa nne mwaka huu kama ulivyopangwa licha ya tishio la mashambulizi ya wapiganaji wa Tuareg.

Rais wa Mali Amadou Toumani Toure
Rais wa Mali Amadou Toumani Toure
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia kituo cha redio ya Taifa, rais Toure amesema kuwa nchi yake imezoea kufanya chaguzi zake hata wakati wa vita kwa hivyo vitisho vya waasi wa Tuareg haviitishi serikali yake dhidi ya kuandaa uchaguzi ulio huru na haki.

Kauli ya rais Toure imekuja kufuatia mapigano yanayoendelea kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo wameendelea kukabilina na vikosi vya serikali huku wakitishia kutwaa miji zaidi na kutishia kuharibu zoezi la uchaguzi.

Wapiganaji wa Tuareg wamekuwa wakishirikiana na kundi la AQMI lenya mafungamano na kundi lla Al Qaeda kuteka nyara wageni kwenye nchi ya Mali, Niger na Mauritania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.