Pata taarifa kuu
KENYA

Mapigano ya kikabila yawakimbiza raia elfu nne kaskazini mwa kenya.

Ripoti ya shirika la kimataifa la msalaba mwekundu imeeleza kuwa zaidi ya watu Elfu nne wameyakimbia makazi yao katika mapigano ya jamii za wakulima na wafugaji kaskazini mwa kenya kutokana na ugumu wa upatikanaji wa huduma za maji na malisho.

Mapigano ya kikabila yalisababisha wakazi wa kaskazini mwa nchi hiyo kukimbilia mpakani mwa Ethiopia.
Mapigano ya kikabila yalisababisha wakazi wa kaskazini mwa nchi hiyo kukimbilia mpakani mwa Ethiopia.
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya Afrika mashariki Alexanda Matheou ametaja maeneo mengi yaliyokimbiwa ni pamoja na moyale,kaskazini mwa nchi ya kenya ambapo zaidi ya wakazi elfu nne waliyahama makazi yao.

Taarifa ya umoja wa mataifa UN iliwahi kusema maelfu ya wakazi wamekimbilia maeneo jirani ya Ethiopia kufuatia mapigano ya kabila la borana na gabra yaliyojiri katika maeneo ya Moyale mpakani mwa Ethiopia.

Kiongozi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya Afrika Mashariki Alexander Matheou amesema haijawahi kutokea kama ilivyotokea moyale shule zote,kijiji chote na vyanzo vya maji viliharibiwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.