Pata taarifa kuu
Mali-Uasi

Waasi wa kundi la MNLA wauteka mji wa Tinzaouatene kaskazini mwa Mali

Hali ya usalama bado ni tete kaskazini mwa Mali hasa kwenye mji wa Tinzauatene mpakani mwa nchi hiyo na Algeria ambapo waaasi wa kundi la MNLA wameuteka mji huo. Mohamed Ag Ghaly mpiganaji wa kundi hilo amethibitisha hilo huku akiahidi kutowa ripoti baadae kuhusu mateka waliokamatwa pamoja na idadi ya wanajeshi wa serikali ya Mali waliouawa katika mapambano.

Wanajeshi wa serikali ya Mali
Wanajeshi wa serikali ya Mali AFP/Kambou SIA
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa serikali ya Mali wamethibitisha mji huo kutekwa na waasi hao, lakini hata hivyo wamesema hapakuwa mapambano, na hakuna mwanajeshi alieuawa, bali wanajeshi waliamuwa kuondoka katika mji huo kuepusha mauaji zaidi ya raia wasiokuwa na hatia na kujipanga vizuri.

Katika mji wa Kidal vyombo vya usalama vinaendelea na harakati zake kuhakikisha usalama na utulivu vinatawala katika mji huo, ulioshuhudia mapambano makali jumalililopita. Hatua kadhaa zilichukukliwa ikiwa ni pamoja na kuzuia myenendo ya nenda rudi, huku wananchi wa mji huo wakikumbwa na hofu kutokana na hali inayo endelea.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.