Pata taarifa kuu

Cote d'Ivoire na Zambia zatinga fainali ya kombe la mataifa ya Afrika

Timu ya taifa ya Cote d'Ivoire itakutana na Zambia kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika itayo chezwa jijini Libreville baada ya timu hizo mbili kushinda mechi zao za nusu fainali.

L'Ivoirien Gervinho.
L'Ivoirien Gervinho. REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Tembo wa Cote d'Ivoire wamefuzu baada ya kuishinda Mali bao 1-0 katika nusu fainali yao iliochezwa mjini Libreville, nchini Gabon. Bao la ushindi la Cote d'Ivoire liliwekwa nyavuni na mchezaji wa Arsenal Gervinho katika kipindi cha kwanza.

Katika Kipindi cha pili, wachezaji wa Mali walijaribu kusawazisha bila mafaanikio, vijana wa Cote d'Ivoire walidhibiti ushindi wao wa bao boja huku wakijaribu mara kadhaa kusindiria msumari bila mafaanikio. Hadi kipenga cha mwisho Cote d'Ivoire iliongoza kwa bao hilo.

Didier Drogba nahodha wa Cote d'Ivoire amewapongeza wenzake kwa mchezo mzuri waliounyesha huku akimsifu sana Gervinho na kusema kwamba amewaokoa. Hata hivyo amewasifu pia vijana wa Aigle wa Mali ambao amesema wameonyesha mchezo mzuri hadi kufikia hatuwa hiyo.

Katika mechi nyingine iliochezwa katika mji wa Bata nchini Gabon Zambia ilikatika matumaini ya Ghana kwenda fainali kwa kuikandika bao 1-0.Bao la Zambia lilifungwa katika dakika ya 78 na mshambuliaji Emmanuel Mayuka.

Katika kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan alikosa kufunga penalti, mlinda mlango wa Zambia akautema nje mpira.
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachezwa siku ya Jumapili mjini Libreville, nchini Gabon, mechi ambayo itatangazwa moja kwa moja kupitia Idhaa ya RFI Kifaransa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.