Pata taarifa kuu
SENEGAL

Rais wa Senegal Wade anasubiri hatima yake iwapo atagombea ngwe ya tatu

Rais wa Senegal Abdoulaye Wade mwenye umri wa miaka 85 sasa na akiendelea kuongoza Taifa hilo kwa miongo kadhaa anasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kujua hatima yake iwapo ataweza kuongoza kwa kipindi cha tatu.

Abdoulaye Wade.
Abdoulaye Wade. RFI / Laurent Correau
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo inasubiriwa huku Vyama Vikuu vya upinzani vikipanga kufanya maandamano makubwa baadaye hii leo kupinga hatua ya Rais Wade kugombea nafasi yake kwa kipindi cha tatu mfululizo.

Baraza la Katiba nchini Senegal ndilo ambalo linatarajiwa kutoa uamuzi na Vyama Vya upinzani vimejiapiza kupiga kambi katika Makao Makuu ya Baraza hilo wakisubiri hukumu ambayo itatolewa.

Serikali imeshapiga marufuku kufanyika kwa maandamano hayo wakihofia kuibuka kwa ghasia ambazo huenda zikafanywa na wafuasi wa Vyama Vya Upinzani wanaoonekana kukerwa na kitendo cha Rais Wade kuendelea kutaka kusalia madarakani.

Msemaji wa Umoja huo wa Vyama Vya Upinzani Alioune Tine amesema maandamano yao yatafanyika kama ambavyo ilivyopangwa licha ya vitisho ambavyo vimetolewa na serikali kupinga maandamano hayo.

Jopo la Majaji watano ndilo ambalo litaamua hatima ya Rais Wade kwenye harakati za kusaka kuwania kiti hicho kwa mara nyingine huku shinikizo kubwa likitaka Kiongozi huyo asuruhusiwe kuvunja katiba.

Wagombea ishirini wa nafasi ya Urais akiwemo Mshindi wa Tuzo ya Muziki ya Grammy Youssou Ndour ni miongoni mwa wale ambao wanasubiri kwa hamu uamuzi huo wa Baraza la Katiba.

Uchaguzi wa Senegal unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ambapo ndiyo hatima ya Uongozi nchini humo utabainika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.