Pata taarifa kuu
NIGERIA

Rais wa Nigeria Jonathan ataka Kundi la Boko Haram liwasilishe madai yao serikalini

Serikali ya Nigeria imelitaka Kundi la Waislam Wenye Msimamo Mkali la Boko Haram ambalo limekuwa likipanga na kutekeleza mashambulizi kujitambulisha na kuweka bayana madai yao kwa serikali ikiwa ni msingi wa kufanya mazungumzo.

REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ndiye ambaye ametoa kauli ya kulitaka Kundi la Boko Haram kujitambulisha wakati huu ambapo takwimu zinaonesha mashambulizi yake yaliuwa watu 500 mwaka 2011 na watu 250 kwenye majuma ya mwanzo ya mwaka huu.

Rais Jonathan amesema iwapo watajitambulisha na kusema ni kwa nini wamekuwa wakitekeleza mashambulizi na kuchangia vifo na kuharibu mali wataketi nao chini kwa ajili ya mazungumzo kushughulikia madai yao.

Kiongozi huyo wa Nigeria amesema serikali yake ipo tayari kuzungumza na Kundi la Boko Haram lakini ni lazima wajue matatizo yao ya msingi ni yepi sambamba na kulifahamu vizuri Kundi hilo.

Janathan amesema serikali yake haiwezi kuacha kusikiliza madai kutoka kwa wananchi wake kwa kuwa hilo ni jukumu lao na iwapo Boko Haram wataainisha madai yao ni wazi yatashughulikiwa kwa wakati.

Rais Jonathan ameongeza kuwa hakuna shaka ya aina yoyote ya kwamba Kundi la Boko Haram linauhusiano na Makundi mengi ya kupigana jihadi ambayo yamekuwa yakitekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga duniani.

Licha ya serikali kusema haijui madai ya Kundo la Boko Haram lakini Kiongozi wake Abubakar Shekau amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa wanataka nchi hiyo itawaliwe kwa sharia za kiislam.

Boko haram limekuwa mstari wa mbele kutaka elimu kutoka mataifa ya magharibi ambayo inatolewa nchini Nigeria iachwe kufundishwa na badala yake sharia za kiislam na elimu ya kiislam ndiyo iwe mbadala.

Rais Jonathan anatoa kauli ya kutaka Kundi la Boko Haram lijitambulishe wakati hu ambapo Kundi hilo kiliendelea kutekeleza mashambulizi yake ambayo yamehamia kwenye Jiji la Kano kwa karibu majuma mawili sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.