Pata taarifa kuu
NIGERIA

Rais wa Nigeria amtimua kazi Mkuu wa Polisi kwa kushindwa kuwadhibiti Boko Haram

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amemtimua kazi Mkuu wa Polizi pamoja na Wasaidizi wake wote sita baada ya kuonekana kushindwa kukabiliana na Mashambulizi yanayofanywa na Kundi la Waislam wenye msimamo mkali la Boko Haram.

Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ambayo imetolewa na Ofisi ya Rais imeeleza kuwa Hafiz Ringim amefukuzwa kazi na nafasi yake imechukuliwa na Mohammed D. Abubakar ikiwa ni hatua za kuendeleza mapambano dhidi ya Kundi la Boko Haram.

Uamuzi huu unakuja wakati huu ambapo mashambulizi ya Kundi la Boko Haram yamezidi kuchacha katika Jiji la Kano na takwimu zinaonesha watu zaidi ya mia mbili na hamsini wamepoteza maisha mwaka pekee kupitia mashambulizi ya kundi hilo.

Rais Jonathan amechukua uamuzi huo mgumu wa kumfuta kazi Mkuu wa Polisi Hafiz kutokana na uwepo wa ukosoaji mkubwa kwa namna ambavyo jeshi nchini humo linakabiliana na Kundi la Boko Haram.

Wananchi wengi nchini Nigeria wanaonekana kutokuwa na imani na jeshi la polisi kutokana na kila kukicha nguvu ya Kundi la Boko Haram kuzidi kukua na kuleta tishio la usalama kwa raia katika Miji mbalimbali.

Tayari serikali imeunda Tume ambayo itakusanya maoni na kutaka kujua ni kwa nini wananchi wamapunguza imani na jeshi la polisi na hivyo kushughulikia dosari ambazo zinaonekana kujitokeza.

Kufukuzwa kazi kwa Mkuu wa Polisi Hafiz kunakuja baada ya kutoroka kwa Mtuhumiwa wa kutekeleza mashambulizi kutoka Kundi la Boko Haram Kabiru Sokoto ambaye alikuwa anashikiliwa na polisi kabla ya kutoka huko Abuja.

Sokoto alitoroka mikononi mwa polisi wakati akihamishwa kutoka kituo kimoja cha polisi kwenda kingine kitu ambacho kilizusha hasira kubwa kwa wananchi ambao walihisi kuna ushirikiano baina ya Kundi la Boko Haram na Jeshi la Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.