Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-UFARANSA

Rais wa Cote D'Ivoire Ouattara aanza ziara nchini Ufaransa

Rais wa Cote D'Ivoire Alassane Ouattara ameanza rasmi ziara yake ya kwanza nchini Ufaransa tangu Vikosi vya nchi hiyo vimsaidie kuingia madarakani mwezi April mwaka jana ambapo anatarajiwa kukusaini makubaliano ya Ulinzi na Rais Nicolas Sarkozy.

Reuters / Bertrand Langlois
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa Ulinzi utakuwa ndiyo agenda kuu katike mazungumzo kati ya Rais wa Cote D'Ivoire Ouattara na Rais Sarkozy tangu nchi hiyo ipitie kipindi kigumu cha umwagaji wa damu baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais.

Ouattara na Sarkozy watasaini makubaliano hayo ya ulinzi siku ya alhamisi wakati wa dhifa maalum ambayo itaandaliwa kwenye Makazi ya Rais wa Ufaransa yanayotambulika kama Elysee.

Ziara hiyo inamaliza mwongo mmoja wa mahusiano yasiyoridhisha kati ya Ufaransa na Mtangulizi wa Ouattara, Laurent Gbagbo ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.

Uhusiano kati ya Ufaransa na Cote D'Ivoire ulianza kuchukua sura mpya baada ya hapo mwaka jana Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa UN na vile vya Ufaransa kushirikiana na wafuasi wa Ouattara kumng'oa Gbagbo.

Rais Ouattara ametengeneza uhusiano mzuri na nchi ya Ufaransa tangu pale ambapo Vikosi vya nchi hiyo vilipomsaidia kumuondoa Gbgabo madarakani baada ya kung'ang'ania madarakana licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi.

Kiongozi huyo wa Cote D'Ivoire Ouattara alivishukuru vikosi vya Ufaransa kwa namna ambavyo waliwasaidia kufanikisha kumuangusha Gbagbo na serikali yake iliyokuwa inatawala kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.