Pata taarifa kuu
KENYA-UHOLANZI

Mahakama ya ICC kuamua iwapo watuhumiwa sita Wakenya wanakesi ya kujibu au la

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC inatarajia kuthibitisha baadaye hii leo iwapo washukiwa sita wanaotuhumiwa kuchangia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 wanakesi ya kujibu au la.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya ICC chini ya Rais wa Majaji Ekaterina Trendafilova ambaye ataongoza jopo la majaji watatu inatarajiwa kuvunja ukimya ya kubainisha iwapo kuna watuhumiwa ambao wanastahili kusimama mbele ya kizimba kujibu mashtaka.

Watuhumiwa hao akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha nchini Kenya Uhuru Kenyatta, Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto na Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu Wa Baraza la Mawaziri Francis Muthaura.

Wengine watatu ambao wanasubiri kujua hatima yao mbele ya Mahakama ya ICC ni pamoja na Mkuu wa Shirika la Posta ambaye alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mohammed Hussein, Waziri wa zamani wa Viwanda Henry Kosgey na Mwandishi wa Habari Joshua Arap Sang.

Ghasia hizo za baada ya uchaguzi zilichangia vifo vya zaidi ya watu elfu moja mia moja huku wengine maelfu wakikimbia makazi yao kuepuka ghasia hizo za baada ya uchaguzi uliomrejesha madarakani Rais Mwai Emilio Kibaki.

Machafuko yalizuka kufuatia Waziri Mkuu wa sasa Raila Amolo Odinga kukataa matokeo ambayo yalimpa ushindi Rai Kibaki na hivyo wafuasio wake kushikwa na hasira na hivyo kuingia barabarani kupinga suala hilo.

Kikao cha Mahakama ya ICC kinatarajiwa kuketi na kisha kutangaza ushahidi ambao utawakuta wale wenye kesi ya kujibu majira ya saa saba na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.

Taharuki imeanza kutanda nchini Kenya huku wananchi wakiwa na shauku kutaka kujua nini hatima ya washukiwa hao sita ambao wamekuwa na nguvu kubwa ya kisiasa na hivyo kubeba wafuasi wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.