Pata taarifa kuu
Mauritania

Serikali ya Mauritania na hati ya kukamatwa kwa mpinzani mkuu Ould Limam Chavi

Serikali ya mauritania imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mpinzani wa rais Mohamed Ould Abdel Aziz, Moustapha Ould Limam Chavi kwa tuhuma za kushirikiana na kundi la kigaidi duniani la al-Qaeda.

Ould Limam Chavi mpinzani mkuu nchini Mauritania
Ould Limam Chavi mpinzani mkuu nchini Mauritania
Matangazo ya kibiashara

Limam Chavi kiongozi mkuu wa upinzani nchini Mauritania anatuhumiwa kwa makosa ya kufadhili na kushirikiana na makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakifanya uhalifu katika ukanda wa Sahel.

Nchi ya Mauritania ilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Burkina Faso kufuatia nchi hiyo kuendelea kumruhusu Ould Limam Chavi kuishi nchini humo kauli ambayo hata hivyo serikali ya Burkina Faso imekanusha na kudai kuwa kiongozi huyo hayupo tena nchini humo na kudaiwa amekimbilia nchini Côte d’Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.