Pata taarifa kuu
Nigeria-Sheria

Mahakama kuu nchini Nigeria yatupilia mbali madai dhidi ya ushindi wa Goodluck Jonatahan

Mahakama kuu nchini Nigeria imetupilia mbali madai dhidi ya ushindi wa rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi wa mwezi April mwaka huu unaodaiwa kuwa na dosari na kutaka urudiwe.

Jaji mkuu nchini Nigeria Aloysius Katsina-Alu.
Jaji mkuu nchini Nigeria Aloysius Katsina-Alu. RFI
Matangazo ya kibiashara

Akitoa tamko la maamuzi ya jopo la majaji saba wa mahakama hiyo jaji Olufunmilayo Adekeye amesema kuwa malalamiko kuhusu ushindi wa rais Goodluck Jonathan hayana ukweli wowote hivyo wameamua kuyatupilia mbali.

Chama cha upinzani cha Congress for Progressive Change CPC kimelalamikia kuwepo kwa dosari katika zoezi zima la upigaji kura mwezi April na kutaka uchaguzi huo ufutwe na ufanyike mwingine.

Kiongozi wa chama hicho na kiongozi wa zamani wa jeshi Muhammadu Buhari ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo amesema kuwa mahakama nchini humo inaendeshwa kisiasa.

Uchaguzi wa urais nchini Nigeria ulisimamiwa na waangalizi ikiwa ni hatua kubwa ya mabadiliko dhidi ya chaguzi zilizopita ambazo zimekuwa zikigubikwa na machafuko na wizi wa kura ingawa matatizo mengine yamesalia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.