Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Chama Cha Rais Ouattara chapata ushindi kwenye uchaguzi wa Wabunge

Chama Tawala Nchini Cote D'Ivoire kinachoongozwa na Rais Alassane Ouattara kimeibuka na ushindi kweny kinyang'anyiro cha uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya jumapili licha ya Chama wa IPFP cha Rais wa zamani Laurent Gbagbo kususia uchaguzi huo.

REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Cote D'Ivoire Youssouf Bakayoko ametangaza matokeo hayo ya mwisho yakinesha kuwa Chama Tawala cha RDR kikipata jumla ya wabunge mia moja na ishirini na saba na kuwashinda wapinzani wao.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa Chama ambacho kinafuatia kwa kuwa na wingi wa viti ni PDCI ambacho kimeungana na Chama Tawala cha RDR kuunda serikali kikipata viti sabini na saba kwenye uchaguzi huo.

Bakayoko amesema Chama Tawala cha RDR kimepata jumla ya asilimia thelathini na sita nukta tano sita ya viti vyote vya ubunge ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na matokeo ya uchaguzi ya mwaka elfu mbili.

Uchaguzi huu unatajwa kuwa ni wenye mafanikio makubwa kuliko ambavyo ilikuwa inatarajiwa na wengi baada ya nchi hiyo kushuhudia uchaguzi wa rais ukichangia kuingia kwenye machafuko.

Chama cha Gbagbo kilisusia uchaguzi huo kwa kile ambacho inasema ni uwepo wa mazingira ya hila na kuchangia uchaguzi huo kutokuwa huru na wahaki tofauti na ambavyo wengi walikuwa wanatarajia.

Gbagbo kwa sasa anashikiliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC akikabiliwa na mashtaka matako ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyotendeka baada ya kung'anga'ania kusalia madarakani licha ya kushindwa uchaguzi.

Takwimu za Umoja wa Mataifa UN zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu tatu walipoteza maisha nchini Cote D'Ivoire kwenye ghasia za baada ya uchaguzi huku wengine maelfu wakikimbilia mataifa mengine kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.