Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge Nchini Cote D'Ivoire kutangazwa hii leo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Cote D'Ivoire inatarajiwa kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge baadaye hii leo huku Chama Tawala cha RDR kikitazamiwa kupata ushindi mnono.

© Reuters/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali yanaonesha chama hicho cha RDR anachotoka Rais Alassane Ouattara kitapata ushindi wa kimbunga kutokana na kuonekana kufanya vizuru kwenye majimbo mengi kwenye uchaguzi huo wa wabunge.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa tayari matokeo ya majimbo mia mbili na ishirini na nane yameshahesabiwa kati ya majimbo yote mia mbili hamsini na tano kwa hiyo wamesalia na kazi ndogo ya kumalizia zoezi hilo.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa Chama Tawala cha Rais Ouattara kimejikusanyia viti mia moja na ishirini na tatu wakati chama cha PDCI kikipata viti tisini na tatu wakati Chama cha Rais wa zamani Laurent Gbagbo cha IPFP kikiambulia viti kumi na viwili tu.

Bado wananchi wa taifa hilo wanasubiri kwa hamu matokeo hayo ya uchaguzi wa wabunge wa kwanza kufanyika tangu kuangushwa kwa Rais Gbagbo ambaye aling'ang'ania kukaa madarakani licha ya kushindwa uchaguzi wa rais.

Chama Cha IPFP tayari kimeshaanza kulalamika na kusema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki na hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi kubatilisha matokeo na kisha kuitisha uchaguzi mwingine.

Chama Cha IPFP cha Gbagbo ambaye kwa sasa yupo katika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ICC akikabiliwa na mashtaka manne yaliyochangiwa na ghasia za baada ya uchaguzi kiligomea uchaguzi huo kabla ya kukata shauri katika dakika za mwishoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.