Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Zoezi la Uhesabuji kura baada ya Uchaguzi wa Wabunge Nchini Cote D'Ivoire laanza

Zoezi la uhesabuji kura za Ubunge nchini Cote D'Ivoire limeanza baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa Bunge tangu kuangushwa kwa Utawala wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Laurent Gbagbo.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo umeshuhudia watu wachache wakijitokeza kwenye zoezi hilo muhimu ambalo lilisusiwa na Chama cha IPFP cha Gbagbo kutokana na kutoridhishwa na maandalizi ya uchaguzi huo.

Chama Cha IPFP kimesema kuwa kulikuwa na upendeleo wa wazi kabisa kwa Chama Tawala cha Rais Alassane Ouattara RDRP ili kiweze kufanikiwa kunyakua ushindi wa viti zaidi vya wabunge.

Chama Cha Gbagbo kimeweka bayana kuwa jeshi la nchi hiyo lilionekana kuwakandamiza wafuasi wao ambao walishiriki kwenye kinyang'anyiro cha kampeni katika taifa hilo.

Rais Ouattara alikuwa ni miongoni mwa wale wananchi wachache ambao walijitokeza kwenye zoezi la upigaji kura naye akasifia hatua ya wananchi kutumia haki yao ya msingi kuchagua wabunge.

Wapigakura wapatao milioni tano walitakiwa kutumia haki yao ya kuchagua wagombea wanaokadiriwa kufikia elfu moja wakiwania viti mia mbili na hamsini na tano vya wabunge nchini Cote D'Ivoire.

Uchaguzi huo umefanyika kwa amani katika maeneo yote ya nchi hiyo hata kwenye kambi ya Gbagbo ambaye kwa sasa yupo kwenye Mahakama Ya Uhalifu wa Kivita ICC akikabiliwa mashtaka matano.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa UN ambavyo vinashika doria nchini Cote D'Ivoire viliendelea na jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye maeneo yote hasa vituo vya kupigia kura.

Uchaguzi huu wa wabunge unatajwa kuwa muhimu zaidi baada ya wananchi wa Cote D'Ivoire kushindwa kuchagua wabunge wao katika kipindi cha miaka kumi na moja wakati wa utawala wa Gbagbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.