Pata taarifa kuu
Cote D' Ivoire

Laurent Gbagbo ailaumu Ufaransa, akana mashitaka

Rais wa zamani wa Cote D'Ivoire Laurent Gbagbo ambaye anakabiliwa na mashtaka manne kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC ameilaumu nchi ya Ufaransa kwa kumshika wakimhusisha na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.Gbagbo alitoa kauli hiyo mara baada ya kupandishwa kwa mara kwanza kwenye Mahakama ya ICC akikabiliwa na makosa manne aliyoyatenda pale alipogoma kuondoka madarakani licha ya kushindwa uchaguzi.

REUTERS/Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Gbagbo amekanusha kuhusika na mashtaka aliyosomewa na mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhailifu wa Kivita, ICC mjini The Hague nchini Uholanzi.

Laurent Gbagbo alifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza akituhumiwa kwa makosa manne ambayo yeye binafsi anawajibika yakiwemo ya mauaji na vitendo vya ubakaji walivyofanyiwa raia wa nchi hiyo katika kipindi cha machafuko.

Mashitaka hayo yanatokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Ivory Coast baada ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 3,000.

Hali ya machafuko ilitokea nchini humo baada ya Gbagbo kugoma kuachia madaraka kufuatia kushindwa na mpinzani wake mkuu Alasane Ouattara katika uchaguzi wa Novemba 2010.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.