Pata taarifa kuu
DRC

Kabila aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa DRC

Tume Huru ya Uchaguzi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI inatarajiwa kutangaza mshindi wa Uchaguzi wa Rais baadaye hii leo baada ya wananchi wa taifa hilo kupiga kura juma lililopita kuchagua kiongozi wanayemtaka.

REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yanasubiriwa wakati yale ya awali yakionesha Rais Joseph Kabila anaongoza kwa asilimia 10 mbele ya mpinzani wake Etienne Tshisekedi.

Etienne Tshisekedi ambaye ndiye mpinzani amekataa matokeo hayo na kuzusha hofu ya kuibuka kwa machafuko na baadhi ya wananchi wameanza kukimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wao.

Matokeo yaliyotangazwa na CENI kunako majira ya saa sita kasoro robo usiku ndiyo yalionyesha kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye anawania nafasi ya urais ambaye pia anatetea nafasi yake Joseph Kabila yuko mbele dhidi ya mpinzani.

Wakati matokeo rasmi yakisubiriwa kutangazwa hii leo kumekuwa na kila jitihada za kidiplomasia kuhakikisha kuwa hakuna uvunjifu wa amani unaoweza kutokea na kusababisha machafuko.

Mwenyekiti wa CENI, Daniel Ngoy Mulunda aliwaambia waandishi wa habari kuwa matokeo hayo mapya yanawakilisha asilimia 67 ya vituo vya kupigia kura ambavyo matokeo yake yameshahesabiwa.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Kabila ana jumla ya kura milioni 5.8 sawa na asilimia 46 ya kura ambazo tayari zimeshahesabiwa wakati Tshisekedi ana kura milioni 4.8 sawa na asilimia 36.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.