Pata taarifa kuu
Cote D' Ivoire

Gbagbo asomewa mashitaka katika mahakama ya ICC, The Hague

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo leo amefikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhailifu wa kivita, ICC mjini The Hague nchini Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Laurent Gbagbo anafikishwa katika mahakama hiyo kusomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza akituhumiwa kwa makosa manne ambayo yeye binafsi anawajibika.

Makosa yanayomkabili Bwana Gbagbo ni pamoja uvunjaji wa haki za binadamu, mauaji na vitendo vya ubakaji walivyofanyiwa raia wa nchi hiyo katika kipindi cha machafuko.

Mashitaka hayo yanatokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Ivory Coast baada ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 3,000.

Hali ya machafuko ilitokea nchini humo baada ya Gbagbo kugoma kuachia madaraka kufuatia kushindwa na mpinzani wake mkuu Alasane Ouattara katika uchaguzi wa Novemba 2010.

Bwana Gbagbo anakuwa mkuu wa nchi wa kwanza wa zamani kusomewa mashitaka katika mahakama ya ICC na leo hatakiwi kujibu shitaka lolote dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.