Pata taarifa kuu
GUINEA YA IKWETA

Asilimia 97 ya Wananchi wa Guinea ya Ikweta waunga mkono mabadiliko ya katiba

Karibu wapiga kura wote wa nchi ya Guinea ya Ikweta wameunga mkono mpango wa rais wa nchi hiyo wa mabadiliko ya katiba, huku upinzani ukidai kuwa mchakato huo ulijawa na udanganyifu.

AFP/Emmanuel Dunand
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo, Clement Nguema amesema asilimia 97 ya watu wamepiga kura kuunga mkono hatua ya kuzuia marais kuhudumu kwa awamu mbili, hata hivyo kifungu hicho kinaelezwa kutomuathiri rais wa sasa.

Rais Teodoro Obiang anayeliongoza taifa hilo ni kiongozi aliyekaa kwa muda mrefu zaidi barani Afrika baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Guinea ya Ikweta inaelezwa kuwa nchi inayoongoza kwa vitendo vya rushwa huku wakosoaji wakisema kuwa mabadiliko ya katiba ni sehemu ya kurudisha imani ya jumuia ya kimataifa.

Katiba mpya haijatanabaisha juu ya obiang kuendelea kubaki madarakani mpaka mwaka 2030 au kujiuzulu baada ya muda wake kuisha mwaka 2016.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.