Pata taarifa kuu
LIBERIA

Raia wa Liberia washiriki duru la pili la uchaguzi hii leo

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa hii leo ikiwa ni siku moja baada ya takriban watu wanne wanaounga mkono upinzani kuuawa baada ya maandamano ya kugomea uchaguzi yalipoitishwa na Winston Tubman.

Raia wa Liberia wakishiriki zoezi la kupiga kura
Raia wa Liberia wakishiriki zoezi la kupiga kura Reuters/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Watu wachache wameonekana kujitokeza kupiga kura ya duru la pili la uchaguzi mjini Monrovia.

Katika duru la kwanza la uchaguzi uliopigwa Mpinzani mkubwa wa rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf aliibuka mshindi wa pili na kuwataka wafuasi wake kutopiga kura za duru la pili la uchaguzi kwa kile alichosema kuwa mzunguko wa kwanza wa uchaguzi ulijawa na udanganyifu.

Wito wa mgomo umekemewa vikali na jumuia ya kimataifa na kuleta hofu juu ya ukuaji wa demokrasia na amani nchini Liberia.

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito saa chache kabla ya kura kuanza kupigwa hii leo kuwa raia wa Liberia lazima wapige kura wakiwa huru, bila woga wowote halikadhalika ametaadharisha watu wachache kutoharibu mchakato wa kisiasa nchini humo.

Obama amesema hatua hii ni fursa kwa Raia kujenga demokrasia thabiti ya nchi yao na kudumisha amani, ustawi na umoja wa kitaifa.

Katika kuhakikisha usalama unadumu hii leo shule kadhaa zinazotumika kuwa vituo vya kupiga kura zimefungwa kwa hofu ya kutokea vurugu zilizojitokeza jana.
Sirleaf aliyeweka historia alipofanikiwa kuwa mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais mwaka 2005, amemshutumu Tubman kwa kukiuka katiba ya nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.