Pata taarifa kuu
TUNISIA

Chama Cha Kiislam Cha Ennahda Cha Nchini Tunisia kimeahidi kuunda serikali katika kipindi cha mwezi mmoja

Chama Cha Kiislam chenye ushawishi mkubwa nchini Tunisia cha Ennahda na kinachoongoza kwenye matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Ubunge nchini humo kimetangaza kitaunda serikali mpya katika kipindi cha mwezi mmoja.

REUTERS/Jamal Saidi
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Chama Cha Ennahda Rached Ghannouchi amesema hawatakuwa na muda wa kupoteza kuunda serikali mpya baada ya kutangaza matokeo ya mwisho kwani ni wazi chama chake kitaibuka na wingi wa kura kwenye kinyang'anyiro hicho.

Chama Cha Ennahda licha ya kutwaa wingi huo wa viti vya wabunge lakini kitahitaji kushirikiana na vyama vingine kuweza kuunda serikali kutokana na kushindwa kupata zaidi ya nusu ya idadi ya wabunge.

Kiongozi huyo wa Ennahda amesema hawatokuwa tayari kuwaangusha wananchi wa Tunisia ambao wamewapa dhamana ya kuongoza kwenye uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia uliokuja miezi tisa baada ya kuangushwa kwa Utawala wa Rais Zine El Abidine Ben Ali.

Matokeo ya awali ya majimbo mia moja na kumi na moja yanaonesha chama cha Ennahda kimefanikiwa kutwa viti arobaini na nne huku nchi hiyo ikiwa na wabunge mia mbili na kumi na saba.

Wabubge hao baada ya kuapishwa na serikali kuanza kazi yake watakuwa na kibarua cha kuandikwa kwa katiba mpya ya nchi hiyo kabla ya kumchangua Rais ambaye ataongoza kwa muda kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi wa rais hapo baadaye.

Wananchi wa Tunisia waliitikia vilivyo hatua ya kuitishwa kwa uchaguzi huo kwani karibu asilimia tisini ya wale waliojiandikisha na kuwa na haki ya kupiga kura walitumia haki yao hiyo vilivyo.

Kufanyika kwa Uchaguzi huo wa Wabunge kunatajwa na Jumuiya ya Kimataifa kama hatua kubwa ya kuelekea kwenye demokrasia ya kweli nchini Tunisia huku mataifa ya magharibi yakipongeza namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.