Pata taarifa kuu
TUNISIA

Chama Cha Kiislam Nchini Tunisia chatangaza kuvuna ushindi

Chama Cha Kiislam chenye ushawishi mkubwa nchini Tunisia Cha Ennahda kimetangaza kina uhakika wa kupata ushindi mkubwa kwenye Uchaguzi wa Wabunge ambao umefanyika siku ya jumapili ukiwa ni Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika katika Taifa hilo tangu kupata Uhuru wake.

REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu umefanyika ikiwa ni miezi tisa tangu kuangushwa kwa Utawala wa Rais Zine El Abidine Ben Ali ambao uliondolewa kutokana na nguvu ya umma kuchoshwa na hali ngumu ya maisha ambayo ilikuwa inawakabili huku ukosefu wa ajira nao ukiwa ni chanzo kikubwa.

Chama hicho cha Kiislam chenye nguvu kubwa kimejitangazia ushindi kwenye uchaguzi huo wa wabunge huku matokeo rasmi ya uchaguzi yakiendelea kusubiriwa kwani hadi mapema jumanne yalikuwa bado hayajatangazwa huku matokeo ya awali yakiwa ushindi Ennahda.

Matokeo hayo ya awali ynaonesha kuwa Chama Cha Ennahda kinaweza kuwa na nguvu kubwa kwenye bunge kutokana na kupata wingi wa viti na tayari Chama pinzani kwao cha PDP kimekubali kuanguka kwenye kinyang'anyiro hicho cha Ubunge.

Kiongozi wa Chama Cha PDP Maya Jribi amesema wanakubaliana na matokeo ya awali ambayo yametangazwa ambayo yanaonesha wameshindwa na wataheshimu maamuzi ambayo yamefanywa na wananchi wa Tunisia.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tunisia inasubiri kwa hamu na wengi kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa wabunge ambapo jumla na nafasi mia mbili na kumi na saba zilikuwa zinagombewa.

Wabunge hao mia mbili kumi na saba watakaochaguliwa wanatarajiwa kuwa na jukumu la kuandaa Katiba Mpya na kisha watateua Rais wa mpito kisha kuandaliwa kwa Uchaguzi wa Rais nchini humo.

Wananchi wengi wa Tunisia walijitokea kwenye kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi kilichofanyika kwa amani na utulivu huku Rais wa Marekani Barack Obama akisema hiyo ni hatua muhimu kwa maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akisema huu ni mwanzo wa utekelezaji wa demokrasia katika nchi ya Tunisia hata mataifa mengine ya Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.