Pata taarifa kuu
Gabon

Maoni tofauti kwa wananchi wa Gabon kuhusu kifo cha mpinzani Pierre Mamboundou

Kumekuwa na maoni tofauti nchini Gabon, baada ya kifo cha mpinzani wa kihistoria Pierre Mamboundou, kiongozi wa chama cha Umoja wa Watu wa Gabon (UPG), ambae aliwahi kugombea urais mara tatu bila kufaulu. Alikufa katika usiku wa Jumamosi kumakia Jumapili akiwa na umri wa miaka 65 kutokana na mshtuko moyo duru za familia zimearifu.

Pierre Mamboundou alieuawa jumamosi usiku Octoba 15, 2011 kutokana na mshtuko wa moyo.
Pierre Mamboundou alieuawa jumamosi usiku Octoba 15, 2011 kutokana na mshtuko wa moyo. AFP PHOTO/Martin VAN DER BELEN
Matangazo ya kibiashara

Kutoweka kwa mpinzani wa kihistoria nchini Gabon Pierre Mamboundou, kiongozi wa chama cha Umoja wa Watu wa Gabon (UPG), aliefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 katika usiku wa Oktoba 15-16, kumezua hisia tofauti kutoka upande wa chama chake na hata upande wa chama tawala.

Fidele Waura, rafiki wa karibu sana na hayati Pierre Mamboundou, ambae ni katibu mkuu wa chama chake, UPG, Umoja wa Watu wa Gabon, amesema kwamba Pierre Mamboundou "alikuwa na muono, alitaka nchi iwe bora. Alikuwa na ndoto kwa wananchi wa Gabon, kuwaletea mabadiliko, ambapo aliwaahidi mabadiliko na kuipata jamuhuri mpya ya Gabon.

Kwa upande wake, Faustin Boukoubi, katibu mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Democratic Gabon, chama tawala amesema, Gabon imempoteza mtu mashuhuri sana mpinzani wa kihistoria, "Alikuwa ni mpinzani halisi, ambae alikuwa hana unafiki, Pierre Mamboundou alikuwa mzalendo halisi.

Kwa upande wake, Rais wa Gabon Ali Bongo amesema Pierre Mamboundou alikuwa mwanademokrasia.

Naye, Zakariya Myboto, kiongozi wa chama cha UGDD, Umoja wa Demokrasia na Maendeleo kwa wananchi wa Gabon amesema kuskitishwa na kifo cha kiongozi wa UPG, na kusema kuwa ni hasara kubwa, kwani alikuwa mtu wa imani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.