Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Mwendesha mashtaka wa ICC Luis Moreno Ocampo kukutana na waathirika wa vurugu za mara baada ya uchaguzi nchini Cote d'Ivoire

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya inayoshughulikia wahalifu wa kivita ya ICC Luis Moreno Ocampo aanza kukutana na waathirika wa vurugu za mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi wa 11 mwaka jana nchini Cote d'Ivoire.

Mwendesha mashtaka wa ICC Luis Moreno Ocampo akisalimiana na rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara alipoonana nae jana
Mwendesha mashtaka wa ICC Luis Moreno Ocampo akisalimiana na rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara alipoonana nae jana AFP / Sia Kambou
Matangazo ya kibiashara

Ocampo amesema kuwa anatarajia kuwasilisha majina ya watu zaidi sita mbele ya majaji wa mahakama hiyo wakituhumiwa kuhusika na machafuko ya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi 11 mwaka jana.

Ocampo ameyasema hayo mara baada ya kukutana na rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara ambapo ataendesha uchunguzi dhidi ya watu ambao wanatuhumiwa kuhusika na uchochezi wa mauaji ya raia zaidi ya 3000 waliouawa ndani ya miezi mitano ya mapigano wakati wa kumuondoa madarakani Laurent Bagbo aliyekuwa rais wa nchi hiyo.

Kuwasili nchini humo kwa mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC kumetokana na amri ya majaji wa katika mahakama hiyo walioagiza kufanyika uchunguzi dhidi ya mauaji ya raia hao ambapo wapiganaji wa Loraa bagbo na wale wa rais Ouattara wanatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umekwishakamilika ambapo kuna majina ya watu ambao anaendelea kuwachunguza kabla ya kuwatangaza kutakiwa kwenda kujibu hoja mbele ya majaji wa ICC.

Mashirika ya kimataifa nchini humo yalitoa taarifa ya pamoja inayoonyesha kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na pande zote mbili, yani wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono Laurent Bagbo na wale wa kiongozi wa sasa Alassane Ouattara.

Rais Ouatttara mwenyewe amekaribisha kwa moyo mkunjufu uchunguzi huo huku akiahidi serikali yake kushirikiana na mahakama hiyo katika kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote ambao watabainika kuwa walihusika na mauaji ya watu hao.

Uchunguzi katika kesi hiyo unatarajiwa kulenga eneo moja la mji wa Duekoue ambako ndiko watu wengi zaidi waliripotiwa kuuawa na vikosi vya Bagbo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.