Pata taarifa kuu
Côte d’Ivoire

Chama tawala zamani nchini Côte d’Ivoire chaahirisha maandamano

Chama cha rais wa zamani wa Cote d'ivoire Laurent Gbagbo kimeahirisha mkutano wake wa hadhara kilichokuwa kimeandaa jumamosi hii jiji Abijan. Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ilikuwa imeomba chama hicho kiahirishe mkutano huo kwa kuhofia ghasia.

EBURNEWS
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa vijana wa chama cha Front Populaire Ivoirien (FPI), Justin Koua amesema kwamba wanaheshimu ombi la serikali. Maandamano hayo walikuwa wameyapanga kufanyika katika Wilaya ya Yopougon kwenye wafuasi wengi wanaomuunga mkono rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent gabagbo

Wakati hayo yakiarifiwa Mkuu wa makahama ya uhalifu wa kivita ICC Louis Moreno Ocampo ambae yu ziarani nchini cotre d'Ivoire amesema atakutana na kundi dogo la watu ambao wanashukiwa kuhusika katika vurumai zilizo tokea nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka uliopita, na iwapo raia wa nchi hiyo wataona umuhimu wa kuwahoji wengine ndipo mahakama itaamua hivyo.

Moreno akampo anakutana leo na mkuu wa tume ya ukweli na maridhiano pamoja na wafuasi wa Laurent Gbagbo baadae atakutana na rais wa chi hiyo allasane Dramane Ouattara kabla ya kuondoka nchini humo

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.