Pata taarifa kuu
Zambia

Rais mteule wa Zambia awataka wawekezaji kutoka Chine kuheshimu sheria ya ajira

Rais mteule wa Zambia Michael Satta ameendelea kutema cheche dhidi ya wawekezaji toka nchini China waliowekeza katika sekta mbalimbali nchini humo kuheshimu sheria ya ajira na kuacha kuwanyanyasa raia wa nchi yake.

Rais mteule wa Zambia Michael Sata wakati akiapiswha mjini Lusaka Septemba 23.2011.
Rais mteule wa Zambia Michael Sata wakati akiapiswha mjini Lusaka Septemba 23.2011. Reuters/Makson Wasamunu
Matangazo ya kibiashara

Rais Satta ameyasema hayo wakati akifanya mazungumzo na balozi wa china nchini Zambia Zhou Yuxiao aliyemtembelea ikulu kwake ameongeza kuwa ni lazima uwekezaji wao uwe wa manufaa kwa raia wa Zambiana unaoheshimu sheria za nchi.

Nchini ya China imewekeza zaidi ya dola bilioni 6.1 sawa na Euro bilioni 4 kusini mwa nchi hiyo, ambapo wawekezaji wake wameingia hofu kufuatia kauli ya rais Satta wakati wa kampeni zake kutishia kuwafukuza nchini wawekezaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.