Michael Sata aapishwa kuwa rais nchini Zambia
Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambia cha Patriotic Front, Michael ameapishwa kuwa rais wa Zambia baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzu wa urais nchini Zambia
Imechapishwa:
Sata alipata asilimia 43 ya kura zilizopigwa na kumshinda Rais Rupiah Banda wa chama tawala cha MMD ambacho kimekuwa mamlakani kwa muda wa miaka 20.
Baada ya jaji mkuu wa nchini Zambia Ernest Sakala kutangaza ushindi wa Sata, zilifanyika sherehe za kuapishwa.
Kulingana na muandishi wa habari wa RFI nchini Zambia Edwin David Ndeketela, watu wawili waliuawa katika eneo linalo kaliwa na wafuasi wengi wa chama cha upinzani.
Watu walijitokeza kwa wingi katika jimbo maafuru kwa uzalishaji Shaba wa Kitwe na Ndola, wamejitokeza na kuvurumisha mawe.
Hasira hizo za wananchi zilichochezwa na hatuwa ya serikali ya kupiga marufu kutangazwa kwa matokeo.