Pata taarifa kuu
SOMALIA-UTURUKI

Waziri Mkuu wa Uturuki aanza ziara yake Somalia kuangalia madhara ya ukame

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili nchini Somalia katika Mji Mkuu Mogadishu kwa ajili ya kujionea uharibifu uliochangiwa na uhaba wa chakula katika eneo la Pembe ya Afrika.

REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Erdogan amezuru kuangalia njaa ambayo inawakabili watu milioni kumi na mbili kutokana na ukame mbaya ulioshuhudia katika eneo hilo kwenye kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita.

Ziara ya Erdogan inamfanya awe Kiongozi wa kwanza kutoka nje ya Bara la Afrika kufika eneo hilo lenye uhaba wa chakula na migogoro ya kisiasa baina ya serikali na Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab.

Erdogan ameambatana na mawaziri wengine wanne ambao miongoni mwa maeneo wanayotarajiwa kuyafikia ni pamoja na Hospital Kuu ya Mogadishu eneo ambalo linawahifadhi watu zaidi ya laki moja.

Somalia inatajwa kama nchi ambayo imeathirika zaidi kwenye eneo la Pembe ya Afrika kwani zaidi ya mikoa mitano katika eneo la Kusini imeathirika zaidi ukichangia na uwepo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ziara ya Waziri Mkuu Erdogan imekuja baada ya kufanyika kwa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kiislam OIC uliofanyika katika Jiji la Istanbul walikoafikiana kutoa dola milioni 350 kukabiliana na ukame na njaa.

Ulinzi mkali umeirishwa nchini Somalia wakati huu ambapo Waziri Mkuu Erdogan ameanza ziara yake wakihofia huenda Wanamgambo wa Al Shabab wakatumia mwanya huo kufanya mashambulizi mapya.

Mapema mwezi huu Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab liliondoa vikosi vyake katika Mji wa Mogadishu wakisema wanajipanga upya kwa ajili ya kuendelea mashambulizi yao dhidi ya serikali ya Rais Sheikh Sharrif Sheikh Ahmed.

Waangalizi wa Chaluka kutoka Umoja wa Mataifa UN wameeleza hali iliyopo nchini Somalia ni mbaya mno hatua inayokuja baada ya mara ya mwisho dunia na Afrika kushuhudia ukame mnamo mwaka 1991- 1992.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.