Pata taarifa kuu
Cote D' Ivoire

Waziri mkuu wa zamani, mtoto wa Gbagbo wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Serikali nchini Cote D'Ivoire imewatia nguvuni washirika wa karibu 12 wa Rais wa zamani Laurent Gbagbo akiwemo mtoto wake na Kiongozi wa chama chake wakiwahusisha na uasi uliofanyika baada ya uchaguzi wa rais.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Mwendesha Mashtaka wa Serikali Noel Dje amesema miongoni mwa mashtaka ambayo yatawakabili washirika hao wa Gbagbo ni pamoja na kushambulia majeshi ya ulinzi sambamba na uasi.
Kukamatwa kwa watu hao kumi na mbili kunafanya jumla ya watu ambao waliokamatwa tangu kuangushwa kwa utawala wa Gbagbo kufikia 38 wakihusishwa na machafuko yaliyosababisha watu zaidi ya elfu tatu kupoteza maisha.
Miongoni mwa watu hao ambao wametiwa mbaroni ni pamoja na mtoto wa Gbagbo, bwana Michael Gbagbo na wanakabiliwa na mashitaka ya kusababisha machafuko ya baada ya uchaguzi nchini humo.
Machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 3000 na watuhumiwa walishukiwa kuhusika wameshikiliwa katika miji tofautitofauti kwa ajili ya kuhojiwa ili kufahamu kama watakuwa na kesi ya kujibu ama la.
Waziri mkuu wa zamani na mshirika wa karibu wa Gbagbo, bwana Pascal Affi N'Guessan naye ni miongoni mwa watu waliokamatwa kuhusiana na tuhuma hizo za kusababisha machafuko na mauaji.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.