Mamadou Koulibaly kiongozi wa muda wa chama cha FPI ajiuzulu na kupania kujiunga na chama kipya
Kiongozi wa muda wa chama cha aliyekuwa rais wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo, Mamadou Koulibaly, ametangaza kujiuzulu kutoka uongozi wa chama chake kwa kuwa viongozi wa chama hicho wamekataa hatua ya kufanya mabadiliko katika chama hicho.
Imechapishwa:
Koulibaly, spika wa bunge la cote d ivoire, aliyekuwa kiongozi wa muda wa chama cha Ivorian People's Front(FPI) baada ya kuanguka kwa gbagbo, amesema anajiuzulu na hivi sasa anataka kujiunga na chama kipya kitakachoitwa Freedom and Democracy for the republic ,wakati huu wakielekea kwenye uchaguzi wa ubunge.
Koulibaly amesema Uongozi wa FPI unaona kuwa kubadilisha mtazamo wa chama ni kuwasaliti wafuasi wa chama hicho waliofungwa na walio uhamishoni.
Koulibaly ameleta mkanganyiko ndani ya chama kwa kukosoa vikali namna ambavyo Ggbagbo alikuwa akijihusisha na machafuko ya kisiasa na mwenendo mzima wa chama kipindi alichokuwa madarakani.