Pata taarifa kuu
Madagascar

SADC yawataka viongozi wa Madagascar kuruhusu kurejea nyumbani kwa rais wa zamani nchini

Ujumbe maalumu toka jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa afrika SADC umeitaka serikali ya Madagascar kumruhusu rais wa zamani wa nchi hiyo Marc Ravalomanana kurejea nyumbani.

Nembo ya  (SADC).
Nembo ya (SADC). (Source : www.sadc.int)
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti anayeongoza ujumbe huo wa SADC unaosimamia kutafuta suluhu ya mgogoro wa nchi hiyo ambaye pia ni rais wa zamani wa Msumbiji Joackim Chisano amesema kuwa ni lazima serikali ya Madagascar imruhusu rais huyo kurejea na pia kumwacha ashiriki siasa za ndani ya nchi.

Ujumbe huo ulikutana na viongozi wa Madagascar wakati wa mkutano wao na viongozi wa baraza la usalama wa Umoja wa Afrika AU mjini Addis Ababa ethiopia kujadili makubalinao ambayo yamefikiwa hadi sasa kati ya rais Andy Rajoelina aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 2009 na mpinzani wake Marc Ravalomanana.

Mwezi wa pili mwaka huu rais Ravalomanana alifanya jaribio la kurejea nchini mwake yeye na familia yake jaribio ambalo hata hivyo lilishindikana baada ya serikali kutangaza kuwa itamkamata pindi akikanyaga ardhi ya Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.