Pata taarifa kuu
Marekani - Somalia

Raia 1 wa Somalia ashtakiwa na mahakama moja ya siri nchini Marekani kwa ugaidi

Mahakama ya siri ya jeshi la marekani imemshtaki raia mmoja wa Somalia ambaye ni kiongozi wa juu wa kundi la Al Shabab kwa tuhuma za kupanga njama za ugaidi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Ahmed Abdulkadiri Warsame alikamatwa mwezi wa nne mwaka huu na vikosi vya marekani na kuhifadhiwa kwa siri katika meli moja ya kijeshi ambako alikuwa akifanyiwa uchunguzi kutokana na tuhumza zinazomkabili.

Mmoja wa maofisa wa marekani waliomuhoji mtuhumiwa huyo wamesema kuwa baada ya kumuhoji kwa zaidi ya siku kumi na nne mtuhumiwa huyo amekiri kushirikiana na kundi la Al Shabab lililopanga njama za kufanya ufaidi mjini New York.

Kesi hiyo ambayo inakuwa ni ya kwanza kuendeshwa kwenye meli ya kijeshi ya Marekani imeelezwa ni miongoni mwa mkakati wa sera ya Rais barck Obama ya kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi bila kufikishwa katika mahakama za kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.