Pata taarifa kuu
Equqtorial Guinea

Mkutano wa AU kuanza leo nchini Guinea Equatorial

Viongozi wa Umoja wa Afrika,wanaanza mkutano wao wa siku mbili leo Alhamisi nchini Equatorial Guinea, mkutano ambao viongozi hao kutoka mataifa ya Afrika wanatrajiwa kuzungumzia hali inavyoendelea nchini Libya na agizo la mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa kivita la kutaka Gaddafi akamatwe na afikishe kizimbani.

Sipop, Mji mpya uliojengwa kwa dhamira ya kuupokea mkutano wa 17 wa viongozi wa nchini wanachama wa Umoja wa Afrika.
Sipop, Mji mpya uliojengwa kwa dhamira ya kuupokea mkutano wa 17 wa viongozi wa nchini wanachama wa Umoja wa Afrika. © AFP / STR
Matangazo ya kibiashara

Inatarajiwa kuwa katika mkutano huo, viongozi hao wanatrajiwa kushikilia msimamo wao wa kumaliza mzozo kati ya serikali ya Gaddafi na waasi kwa njia ya mazungumzo.

Mbali na mgogoro wa libya, viongozi hao pia wanatarajiwa kuzungumzia uhuru wa Sudan Kusini unataitarajiwa kufanyka tarehe tisa mwezi ujao wa Saba, na kuona namna ya kudumisha uhusiano bora kati ya sudan Kaskazini na Kusini,hasa kuhimiza amani katika eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta.

Raia wa Sudan walipiga kura ya kujitenga Kaskazini mwezi Januari mwaka huu, kutokana na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya viongozi wa sudan Kusini na Kaskazini mwaka wa 2005 huko Nairobi nchini Kenya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.