Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI

Mjumbe maalumu wa Urusi mbioni kuelekea Tripoli, Libya

Mjumbe maalumu toka nchini Urusi aliyetumwa na rais Dmitry Medvedev kwenda kujaribu kutafuta suluhu nchini Libya amemamliza ziara katika ngome ya waasi ya Benghazi na kuwa sasa anajiandaa na safari ya kuelekea mjini Tripoli.

Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Libya  Khaled Kaim ambaye atakutana na ujumbe wa Urusi
Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Libya Khaled Kaim ambaye atakutana na ujumbe wa Urusi Reuters/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe huyo Mikhail Margelov amewaambia waandishi wa habari mjini Moscow mara baada ya kurejea toka nchini Libya, kuwa amefanya mazungumzo na upinzani nchini humo na sasa anaandaa safari ya kurejea nchini humo kuelekea mjini Tripoli.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya rais Medvedev ujumbe huo ukielekea mjini Tripoli hautakutana na kiongozi wa Libya Kanali Moamer Gaddafi na badala yake wataonana na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Libya.

Kuhusiana na kushinikizwa kutolewa madarakani kwa kanali Gaddafi mjumbe huyo amesema kuwa hilo ni swala ambalo lipo mikononi mwa Kanali mwenyewe akisema kuwa ni lazima kiongozi huyo afanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa baadae wa taifa la Libya.

Kuhusu safari ya kuelekea mjini Tripoli kiongozi huyo hakuweka bayana ni lini ujumbe wake utaelekea nchini humo na kudai kuwa wanasubiri maandalizi ya NATO kufanywa kuhusiana na usalama ili kuhakikisha hakuna kibaya kitakachotokea wakati wa safari hiyo.

Bwana Margelov amesema kuwa hali inavyoonekana kwa sasa ni wazi kuwa bado kuna nafasi ya viongozi wa Libya kumaliza tofauti zao na kusema kuwa anasubiri akutane na viongozi wa serikali na kufanya nao mzungumzo kujua namna ya kumaliza mzozo uliopo nchini Libya.

Wakati ujumbe huo ukiwa katika harakatiza kutafuta suluhu shinikizo zaidi la kumtaka kanali Gaddafi ang'atuke madarakani limeendelea huku umoja wa nchi za kiarabu ukiahidi kuwasadia waasi kiasi cha fedha cha zaidi ya dola milioni 500.

Hiyo jana wakati wa mkutano huo, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Bi Hillary Clinton alisisitiza kuwa siku za kiongozi huyo kukaa madarakani zinahesabika na kutoa wito kwa kiongozi huyo kuondoka madarakani kwa hiari yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.