Pata taarifa kuu
UGANDA

Rais wa Uganda aapishwa kuongoza awamu ya nne

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameapishwa kuongoza taifa hilo kwa kipindi cha nne huku akiahidi kuendelea kushirikiana na mataifa jirani sambamba na kuhahakikisha uchumi wa taifa lake utaendelea kustawi huku akiapa kuilinda na kuitekeleza katiba ya nchi hiyo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa katika shughuli zake za kiserikali
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa katika shughuli zake za kiserikali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 66 amekaa madarakani tangu mwaka 1986 amesema atahakikisha utawala wa sheria unatekelezwa katika nchi hiyo katika kipindi chake cha awamu ya nne.

Museveni amekula kiapo mbele ya marais Kenya, Mwai Kibaki, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Robert Mugabe wa Zimbabwe ambao wamehudhuria sherehe hizo ambazo zimehushuhudiwa na mamia ya wananchi.

Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa Rais Museveni amesema taifa hilo litaendelea kushirikiana na Sudan Kusini ambayo imejitenga kutoka Kaskazini ambayo iliwakilishwa na Kiongozi wake Silva Kiir.

Rais Museveni ametangaza mpango wa nchi hiyo kuanza uchimbaji wa mafuta kwenye taifa hilo hatua ambayo inaweza kusaidia kuongeza pato la taifa katika miaka ijayo.

00:54

Rais Yoweri Kaguta Museveni akitaja vipaumbele katika serikali yake

Kiongozi huyo hakusita pia kugusia tatizo elimu ya juu ambapo ameweka bayana watahakikisha migomo kwenye vyuo vikuu inapatiwa dawa na kukomesha ili wanafunzi watumie muda mwingi kwenye masomo.

Rais Museveni kwenye sherehe hizo alipokea heshima za kijeshi katika shughuli hiyo ambayo imefanyika katika Viwanja vya Kampala ambapo vikundi vya ngoma navyo vilipamba shughuli hiyo.

Katika hatua nyingine maelfu wa wafuasi wa Kiongozi wa Upinzani Dokta Kizza Besigye walijitokeza kumpokea wakati akirejea kutoka nchini Kenya ambapo alikuwa anapatiwa matibabu ya macho.

Dokta Besigye amekiri kufurahishwa na mapokezi ambayo ameyapata na ameahidi kuendelea na kmapeni zake za kuishinikiza serikali kushughulikia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

Kiongozi huyo wa Chama Cha FDC akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ameshuhudia wafuasi wake wakiimba kuwa yeye ndiye ambaye anastahili kuapishwa kuchukua wadhifa wa urais wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.