RFI Katuni za Meddy

Katuni hizi zinashiria yale yanayoendelea kushuhudiwa ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kinyume cha sheria mwandishi wa habari wa RFI katika lugha ya Haousa nchini Cameroon Ahmed Abba.

Eritrea na Ethiopia zafunua ukurasa mpya baada ya kukubaliana kusitisha vita vya miaka 20, Julai 11, 2018.

Kodi mpya kwa watumiaji wa mitandano ya kijamii nchini Uganda, 05 Julai, 2018.

USA-EU: Hatua za ulipizaji kisasi kwa kodi ya Marekani kuhusu uagizaji wa bidhaa za chuma na bati, Juni 26, 2018.

Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi: Idadi ya wakimbizi inaendelea kuongezeka duniani kote, Juni 20, 2018.

Kim / Trump wajadiliana kuhusu mkataba wa nyuklia, Juni 12, 2018.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara ya kikazi Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kushawishi nchi hizi Ulaya kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, Juni 6, 2018.

Kenya yapambana dhidi ya Rushwa wakati ambapo mamilioni ya dola yalizoibiwa kutoka Shirika la huduma kwa vijana (NYS), Mei 31, 2018.

Raia wa DRC wakiwa katika "vifungo viwili" katika mabega yao: Virusi vya Ebola na makundi yenye silaha yanayoendelea kuwa tishio. 24/05/2018

Burundi: Marekebisho ya Katiba yatashuhudia rais Pierre Nkurunziza akisalia madarakani hadi mwaka 2034. 17/05/2018

USA/Iran: Ingawa jumuiya ya kimataifa imefikia makubaliano na Iran ya kuacha uzalishaji wa vifaa vya nyuklia kwa matumizi ya kijeshi, Donald Trump ajitoa kwenye mkataba huu, Mei 9, 2018.

Siku ya kimataifa ya wafanyakazi, Mei 1, 2018.

Licha ya juhudi za bara la Afrika kutokomeza ugonjwa wa Malaria, bado ugonjwa huo unaua mamilioni ya raia

Kibonzo hiki kinaelezea uhuru wa matumizi wa mitandao ya kijamii ulivyo katika hatari ya kumomonyoka nchini Tanzania na Uganda.

Shambulio la kemikali nchini Syria laibua mvutano kati ya nchi za Magharibi na Urusi, Aprili 12, 2018.

Kim Jong UN alifanya ziara ya kushtukiza kwa Rais wa China Xi Jinping mwishoni mwa mwezi Machi wiki chache tu kabla ya mkutano na Marekani na Korea Kusini.

Kigali Mkutano wa AU: Nigeria yaonesha kutokuwa tayari kutia saini mkataba wa biashara huru kwa bara la Afrika. 21.03.2018

Kibonzo hiki kinaelezea rais wa Tanzania John Magufuli akiwaonya waaandamanaji kuwa serikali itakabiliana nao iwapo watajaribu kuandamana kuipinga serikali yake matamshi aliyotoa Machi 9 2018

Hayo ni miongoni mwa yale wanawake wanayokabiliana nayo katika maisha yao, Machi 8, 2018.

Marekebisho ya kikatiba Burundi: ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa kura ya "hapana".

Wakimbizi wa DRC nchini Rwanda wanalalamika kuhusu mazingira yao ya maisha, Februari 22, 2018.

Afrika Kusini: Jacob Zuma, aliepotza imani ya chama chake, ajiuzulu, Februari 15, 2018.

Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka chama chake cha ANC, sasa yuko njia panda, akishikilia kamba nyembamba, Februari 7, 2018.

Raila Odinga ,mwanasiasa wa upinzania, aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais alijiapisha mapema wiki hii kama raia wa wananchi wa Kenya, Januari 31, 2018.

Utawala wa Kabila nchini DRC unakabiliwa na maandamano kwa wito wa Kanisa Katoliki, Januari 25, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump hana imani na nchi za Kiafrika, Januari 18, 2018.

Korea ya Kaskazini yakubali mazungumzo na Korea Kusini, Januari 11, 2018.

Korea ya Kaskazini: Trump anadai kuwa na "kitufe kikubwa na chenye nguvu zaidi ya nyuklia", Januari 4, 2018.

Nyota wa zamani wa soka George Weah ameshinda uchaguzi mkuu wa rais kwa kura nyingi, Desemba 28, 2017.

Baada ya kutumikia kifungo cha zaidi ya miezi 29, hatimaye mwanahabari wa RFI idhaa ya Hausa Ahmed Abba sasa atakuwa huru, Desemba 22, 2017.

Hatimaye wabunge wa Uganda wamepitisha muswada wa mabadiliko ya katiba kuondoa kipengele cha ukomo wa umri wa mtu kuwania urais, sasa rais Yoweri Museveni yuko huru kuwania uchaguzi ujao, Desemba 20, 2017.

Mizozo ya kivita nchini DRC inasababisha sio tu mdororo wa usalama, bali pia njaa kwa raia, Desemba 14, 2017.

Vita vya maneneo vyaongezeka kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Desemba 6, 2017.

Biashara ya Binadamu nchini Libya yatia wasiwasi Umoj awa Ulaya (EU), Novemba 29, 2017.

Zimbabwe: Baada ya Mugabe kujiuzulu Emmerson Mnangagwa  achukua madaraka, Novemba 22, 2017.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anaamini kuwa bado ni kiongozi halali wa Zimbabwe na kupinga shinikizo kutoka kwa jeshi linalotaka kumuondoa mamlakani, Novemba 16, 2017.

Maandamano ya upinzani nchini Togo yanaendelea, licha ya wito na makataa ya Serikali kuyapiga marufuku. Upinzani umeendelea kupinga utawala wa rais Faure Gnassingbe, Novemba 10, 2017.

Maandamano makubwa mashariki mwa DRC kushinikiza Rais Kabila kuandaa uchaguzi wa urais ambao ungelifanyika mwishoni mwa mwaka 2016, Novemba 2, 2017.

Mzozo wa Catalonia kuhusu uhuru wa eneo hilo umekua ni mzigo wa matatizo kwa Umoja wa Ulaya, Oktoba 26, 2017.

Amkani hali si shwari tena Somalia baada ya kushuhudia shambulio baya zaidi la bomu kuwahi kutekelezwa mjini Mogadishu, Oktoba 18, 2017.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ajiondoa katika uchaguzi wa Oktoba 26, Rais Uhuru Kenyatta na Tume ya Uchaguzi (IEBC) wanasema uchaguzi utafanyika Oktoba 26 kama ilivyopagnwa, Oktoba 12, 2017.

Marekebisho ya katiba kuondoa kipengele cha ukomo wa umri wa rais yamezua hali ya sintofahamu nchini Uganda, Oktoba 6, 2017.

Rais Magufuli ameagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani, nae Donald Trump aagiza kujengwa ukuta na mpaka na Mexico, Septemba 28, 2017.

Aung San Suu Kyi atakiwa kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba Rohingya, Septemba 21, 2017.

Rais wa Marekani Donald Trump alijiondoa kwenye makubaliano ya Paris kuhusu badiliko ya tabia nchi, lakini ameanza kujuta baada ya nchi yake kukumbwa na kimbunga Irma. Septemba 14, 2017.

Mahakama Kuu ilifuta matokeo ya uchauzi wa urais nchini Kenya, Septemba 7, 2017.

Kiongozi wa Korea Kaskazini anadharau jumuiya ya kimataifa kwa kuendelea kurusha makombora ya masafa marefu, Agosti 31, 2017.

Rais wa Marekani Donald Trump atangaza mkakati mpya wa vita nchini Afghanistan, Agosti 24, 2017.

Matamshi makali kati ya rais wa Marekani na Korea Kaskazini yapungua, Agosti 17.

Uhuru Kenyatta ashinda uchaguzi kwa mara ya pili mfululizo ( 2013/2017), Raila Odinga alalamika, Agosti 13, 2017.

Nchini Kenya, wapiga kura wanapiga kura,wanataka amani lakini wana hofu, Agosti 7, 2017

Uturuki yashutumiwa kwa kuminya uhuru wa Vyombo vya Habari, Agosti 1, 2017.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro anakabiliwa na shinikizo la upinzani kutakiwa kuondoka madarakani, Julai 20, 2017.

Serikali ya DR Congo inatangaza kuwa uchaguzi utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka 2017, Julai 12, 2017.

USA/Iran: Ingawa jumuiya ya kimataifa imefikia makubaliano na Iran ya kuacha uzalishaji wa vifaa vya nyuklia kwa matumizi ya kijeshi, Donald Trump ajitoa kwenye mkataba huu, Mei 9, 2018.

Donald Trump na matumizi yaliyopindukia ya mitandao ya kijamii anayotumia kujibu wakosoaji wake, Julai 4, 2017.

Vita na machafuko barani Afrika vyasababisha watu kukimbilia nchi jirani, Juni 25, 2017.

Rais Magufuli na vita dhidi ya makampuni ya madini yaliyokwepa kodi, Juni 17, 2017.

Rais wa Marekani Donald Trump hakubaliani na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Juni 7, 2017.

Vita vya maneno kati ya Korea Kaskazini, Marekani, Urusi na Umoja wa Mataifa, Mei 31, 2017.

DRC inakabiliwa na virus vya Ebola na migogoro ya kisiasa, Mei 26, 2017.

Uchunguzi kuendeshwa na Donald Trump pamoja na Urusi, Mei 21, 2017.

Ushindi wa Emmanuel Macron Mei 15, 2017.

Ushindi wa Emmanuel Macron Mei 8, 2017.

Ahmed abba, mwandishi wa RFI katika lugha ya Haousa nchini Cameroon kizuizini, Aprili 28, 2017.

Ahmed abba, mwandishi wa RFI katika lugha ya Haousa nchini Cameroon ahukumiwa kifungo cha miaka 10, Aprili 24, 2017.

Ahmed abba, mwandishi wa RFI katika lugha ya Haousa nchini Cameroon kizuizini, aprili 15, 2017.