Pata taarifa kuu
JAPAN-NISSAN-GHOSN-UCHUMI

Nissan yamdai Carlos Ghosn euro milioni 83

Kampuni ya magari ya Japani, Nissan, imewasilisha mashtaka katika mahakama ya kiraia nchini Japan dhidi ya Carlos Ghosn, kiongozi mkuu wa zamani wa makampuni ya magari Nissan na Renault, kwa makosa na shughuli za ulaghai. Nissan inadai fidia ya dola milioni 90, sawa na zaidi ya euro milioni 83,400,000 .

Kiongozi wa zamani wa makampuni ya magari Renault-Nissan Carlos Ghosn katika mkutano na waandishi wa habari Beirut, Lebanon, Januari 8, 2020.
Kiongozi wa zamani wa makampuni ya magari Renault-Nissan Carlos Ghosn katika mkutano na waandishi wa habari Beirut, Lebanon, Januari 8, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Kiwango hiki kinaweza kupanda zaidi, Nissan imebaini kwamba malipo ya kudai 'fidia' yanapaswa kuongezeka katika siku zijazo.

Nissan inasema kulingana na matokeo ya ukaguzi wa ndani uliochapishwa mwezi Septemba na ambayo yanaonyesha kwamba kiongozi huo wa makampuni hayo mawili, alitumia dola milioni 27 kutoka kwa kampuni kanzu ya Nissan kwa kununua makazi ya kifahari huko Beirut na Rio de Janeiro kwa matumizi pekee ya kibinafsi.

Nissan pia inamshutumu Carlos Ghosn kwa kuwa alimlipa dada yake dola 750,000 kwa mkataba wa mshauri hewa, lakini pia kwa kuwa alitoa pesa milioni mbili kwa fedha za kampuni hiyo kwa vyuo vikuu vya Lebanon, bila vithibitisho vyovyote vile, au kutumia ndege za NIssan kwa matumizi yake binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.