Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Mdororo wa uchumi duniani na migogoro ya kimataifa kugubika mkutano wa G7 Biarritz

media Jengo ambako kutafanyika mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani (G7) Biarritz, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Agosti 2019. REUTERS/Regis Duvignau

Nchi za zilizostawi kiuchumi duniani (G7) zinakutana katika mji wa Biarritz kusini magharibi mwa Ufaransa kuanzia Agosti 24 hadi 26, wakati uchumi wa dunia unaendelea kushuka na machafuko mengi, hasa barani Asia, vinaendelea kuzua mvutano wa kimataifa.

Ukuaji wa chini, kushindwa kulipa madeni mbalimbali, kuzorota kwa zoezi la kutoa mikopo, gawio la chini ...vyote hivyo vinatarajiwa kuzungumziwa katika mkutano wa nchi ziliostawi kiuchumi duniani (G7). Uchumi wa Uingereza na Ujerumani, mabingwa wa Ulaya kwa uchumi wa kiwango cha juu, ulianza kupanda katika msimu wa pili wa mwaka.

China, uchumi wake umepungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kwamba shughuli ya uingizaji bidhaa nchini imekuwa dhaifu. Nchini Marekani, kiwango cha uzalishaji kimeshuka mara mbili mwezi huu. Yote hayo ni dalili zinazoonyesha kuwa uchumi duniani umeshuka.

Mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani, lakini pia kati ya Ulaya na Marekani umeongeza dosari katika kushuka kwa uchumi duniani na hivo kuweka mashaka mengi kuhusu mauzo ya nje, na pia nia ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Lakini viongozi wa kisiasa kutoka nchi zilizostawi kiuchumi (G7) na wamiliki wa makampuni makubwa kutoka nchi hizo wanaweza kwenda mbali zaidi ya yale waliyokuwa wamekubali kuunga mkono uchumi: Tume ya Ulaya haijawahi kuwa makini kuhusu nakisi ya bajeti na viwango vya riba bado ni vya kiwango cha chini kabisa, miaka kumi baada ya mdororo wa ya fedha na kiuchumi.

Wadadisi wanasema mdororo wa uchumi wa kimataifa unaumiza zaidi nchi maskini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana