Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-SIASA

Idara ya ujasusi yaomba kufanyika ukaguzi wa matumizi ya fedha kwenye wizara mbalimabli DRC

Idara ya ujasusi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (ANR) imetaka ukaguzi ufanyike kwenye wizara mbalimbali nchini humo. ANR imetaka ukaguzi huo ufanyike tangu mwezi Januari, mwezi ambao Felix Tshisekedi alitawazwa kama rais mpya wa nchi hiyo.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakati wa ziara yake Washington, Aprili 3, 2019.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakati wa ziara yake Washington, Aprili 3, 2019. © ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika barua inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, mkuu wa idara ya ujasusi ameomba kufanyiwa ukaguzi fedha zote zilizotumiwa na wizara mbalimbali tangu kutawazwa kwa rais Felix Tshisekedi mwezi Januari mwaka huu.

Barua hiyo iliyo na jina la ANR iliandikwa tarehe 17 Agosti. Mkuu wa idara ya ujasusi Justin Inzun Kakiak, amemwagiza Mkaguzi Mkuu wa Fedha kukagua " fedha zote zilizotumiwa na wizara mbalimbali tangu kuapishwa kwa Rais Felix Tshisekedi ".

Kwa wiki kadhaa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wamekuwa wakilaani kukithiri kwa ufisadi katika wizara mbalimbali nchini DRC. Hivi karibuni Wizara ya Masuala ya Jamii ilitumia dola 600,000 kwa operesheni ya kibinadamu katika mkoa wa Kivu Kusini. Lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yanaona kwamba fedha hizo hazikuwafikia walengwa, na zimewekwa kwenye akaunti binafsi mjini Kinsahsa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.