Pata taarifa kuu
DUNIA-IMF-UCHUMI

Ripoti ya IMF: Ukuaji wa uchumi waendelea kudorora

Ripoti mpya ya robo mwaka kuhusu uchumi wa dunia inayotolewa na shirika la Fedha Duniani, IMF, imeonesha ukuaji mdogo wa uchumi kidunia huku ikionya kuhusu vita vya kibiashara, uwezekano wa kukosekana kwa mkataba wa Brexit na changamoto nyingine vinachangia kudorora kwa ukuaji wa uchumi.

IMF inasema uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo.
IMF inasema uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ripoti yake, IMF inasema kuwa mizozo ya kibiashara imepunguza kasi ya uwekezaji na kudorora kwa sekta ya viwanda, IMF ikitoa wito kwa mataifa kutotumia tozo kumaliza tofauti zao.

IMF sasa inasema uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo ambapo katika mwaka 2019 uchumi wa dunia unatarajiwa utakuwa kwa asilimia 3.2 na asilimia 3.5 kwa mwaka 2020.

Aidha shirika hilo limesema ikiwa hali ya sasa itaendelea kushuhudiwa mfululizo, basi huenda mambo yakawa mabaya zaidi kwa mataifa mengi na hasa yale yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.