Pata taarifa kuu
G20-OSAKA-TABIANCHI-UCHUMI-BIASHARA

G20 Osaka: Vigogo wa dunia wakutana Osaka, Japan

Mkutano wa kilele unaojumuisha nchi zilizostawi kiviwanda na kiuchumi, G20, umeanza katika mji wa Osaka, nchini Japan leo Ijumaa Juni 28, 2019.

Maandalizi ya picha kwa viongozi wanaoshiriki mkutano wa G20, Osaka, Japan, Juni 28, 2019.
Maandalizi ya picha kwa viongozi wanaoshiriki mkutano wa G20, Osaka, Japan, Juni 28, 2019. REUTERS/Kim Kyung-Hoon/Pool
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa dunia wamekusanyika nchini Japan kushiriki katika mojawapo ya mikutano ya nchi za G20 yenye migawanyiko mikubwa kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi.

Vita vya kibiashara vinavyoendelea kati ya Marekani na China, mivutano ya siasa za kimaeneo na mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa mada kuu. Mkutano huo utatawaliwa na masuala ya kibiashara, huku wengi wakisubiri kuona kama rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping wanaweza kufikia makubaliano ya mzozo wao ambao umekuwa na athari mbaya kwa uchumi wa ulimwengu.

Hata hivyo mkutano huu unatabiriwa kwamba utazingatia zaidi siasa za mataifa hayo kuliko maswala ya kidiplomasia ya kimataifa.

Akizungumza leo mwanzoni mwa mkutano huo, Trump amesema kuwa atajadili biashara na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika mazungumzo yake pembezoni mwa mkutano huo wa G20 .

Aidha amesema kuwa hana haraka katika kuutatua mzozo kati ya Marekani na Iran.

Kuhusu China na Marekani, rais wa China Xi Jinping atasisitiza kuepukwa kwa mijadala kuhusu masuala ya ndani ya nchi yake hasa kuhusiana na mgogoro wa Hongkong juu ya mswada wa sheria wa wahalifu kupelekwa katika mahakama za China. China ilisema haitaruhusu maandamno ya Hongkong kujadiliwa katika mkutano huo wa G20 japo kunatarajiwa kufanyika maandamano nje ya majengo kunakofanyika mkutano huo.

Kwa upande mwengine rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kuwa kama hakutakuwa na ahadi tosha na kamilifu kuhusu tabianchi, Ufaransa haitoweka saini kwenye tangazo la mwisho la mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.