Pata taarifa kuu
LIBYA-UCHUMI

Takriban makampuni 40 ya Ulaya yasimamishwa kutoa huduma Libya

Libya imechukuwa uamuzi wa kusimamisha shughuli za baadhi ya makampuni arobaini ya Ulaya yanayotoa huduma nchini humo. Sheria hii ya kurasa 4 imechapishwa na kutolewa kupitia vyombo vya habari Alhamisi 9 Mei.

Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya (GNA) Fayez al-Sarraj akifanya ziara barani Ulaya ambapo Mei 7, 2019alizuru Roma na Berlin, Mei 8 Paris na Mei 9 London.
Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya (GNA) Fayez al-Sarraj akifanya ziara barani Ulaya ambapo Mei 7, 2019alizuru Roma na Berlin, Mei 8 Paris na Mei 9 London. © Filippo MONTEFORTE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makampuni haya yanashtumiwa kwamba hayakusajilisha upya vibali vyao ili kuendelea na shughuli zao nchini Libya.

Makampuni kadhaa ya Ufaransa na Ujerumani ni miongoni mwa makampuni hayo yaliyosimamishwa kuendelea kutoa huduma nchini Libya. Total, kampuni ya mafuta ya Ufaransa iko kwenye nafasi ya mwanzo ya orodha ya makampuni yaliyosimamishwa. Kampuni ya Siemens kutoka Ujerumani na kampuni ya mawasiliano ya simu ya Alcatel-Lucent, ni miongoni mwa makampuni hayo yaliyosimamishwa kutendelea kutoa huduma.

Sheria hiyo ilitiliwa saini na Ali Issaoui, Waziri wa Uchumi na Viwanda wa Libya.

Sheria hii haikusudii kuvunja uhusiano na makampuni haya, lakini inawataka kuheshimu sheria, taarifa kutoka Wizara ya Uchumi na Viwanda imesema, huku ikiyataka makampuni hayo kuchukua hatua za kujiweka sawa kwa kufuata sheria ya Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.