Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Marekani: China imerudi nyuma kwa kutozingatia ahadi zake

China imerudi nyuma kwa kutozingatia baadhi ya ahadi zake katika mazungumzo ya biashara na Marekani, na kusababisha Donald Trump kutishia kuweka ushuru mpya kwa bidhaa kutoka China chanzo cha serikali ya Marekani ambacho hakikutaja jina, kimesema.

Rais Donald Trump anatoa hotuba yake karibu na bendera za Marekani na China katika mkutano na Rais Xi Jinping na wajasiriamali, Beijing Novemba 9, 2017.
Rais Donald Trump anatoa hotuba yake karibu na bendera za Marekani na China katika mkutano na Rais Xi Jinping na wajasiriamali, Beijing Novemba 9, 2017. REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House iko tayari kuendelea na mazungumzo kama China itabadili msimamo, Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin na Mwakilishi wa Biashara Robert Lighthizer wamewaambia waandishi wa habari Jumatatu wiki hii

"Karibu mwishoni mwa juma lililopita tuliona kuwa (...) China imerudi nyuma kwa ahadi zake," Robert Lighthizer amesema, huku akiongeza kuwa hatua hiyo ya China imesababisha mabadiliko makubwa kwenye makubaliano yaliyofikiwa.

"Kwa mtazamo wetu, hiyo haikubaliki," amesema Robert Lightizer.

Ujumbe wa China utakuwa Washington Alhamisi na Ijumaa wiki hii kuendelea na mazungumzo, na Lighthizer amesema wanatarajia kuwa Naibu Waziri Mkuu wa China Liu.Donald atahudhuria mazungumzo hayo.

Trump anataka makubaliano yanayohusiana na mabadiliko makubwa ya miundo katika mahusiano ya biashara na China, jambo ambalo halipo wakati huu, Lightizer ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari na Steven Mnuchin.

Rais wa Marekani alitangaza Jumapili kuwa dola bilioni 200 za bidhaa kutoka China ambazo hapo awali zilikuwa zikitozwa ushuru wa asilimia 10 zinapoingizwa nchini Marekani zitatozwa asilimia 25 kuanzia Ijumaa.

Steven Mnuchin amesema itasikitisha ikiwa nchi hizo mbili hazitofikia mkataba wakati walikuwa na matumaini ya kufikia mkataba mwishoni wa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.