Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHUMI-JAMII

Emmanuel Macron aelezea hatua ya pili ya muhula wake wa miaka mitano

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa majibu yake kwa vyombo vya habari katika mjadala mkubwa uliofanyika Alhamisi hii, Aprili 25, kujaribu kuzima maandamano ya "vizibao vya njano" na kuzindua upya muhula wake wa miaka mitano mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano  na waandioshi wa habari baada ya mjadala mkubwa, katika ikulu ya Elysee, Paris, Aprili 25, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandioshi wa habari baada ya mjadala mkubwa, katika ikulu ya Elysee, Paris, Aprili 25, 2019. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron ameelezea mwelekeo wa hatua ya muhula wake wa miaka mitano.

Mjadala huo uliohudhuriwa na waandishi wa habari takribani 300 ulidumu saa mbili na nusu.

Kwanza, Emmanuel Macron alionyesha nia yake ya kuwatuliza nyoyo wananchi wa Ufaransa, akitaka "kujenga upya mradi wa kibinadamu," amesema. Kwa mujibu wa rais Macron, "mgogoro wa vizibao vya njano umenibadilisha". "Nimeweza" kuwa "jasiri", "wakati mwingine sikutenda haki na ninajutia hilo".

Rais ameelezea hatua zake, na kauli yake ya "ubinadamu", ili kukabiliana na "kiburi" ambacho wengi walimshtumu wakati wa maandamano ya "vizibao vya njano".

Hata hivyo rais Emmanuel Macron hakutoa ahadi nyingi kwa maandamano ya "vizibao vya njano".

Kwa upande mwingine, waandamanaji "wa vizibao vya njano", wamefutilia mbali hoja ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu jitihada za kijamii, lakini wamependekeza kuwepo na kura ya maoni rahisi na hakuna kurejelea mageuzi ya kodi ya utajiri (ISF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.