Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Sudan: Fedha nyingi zakamatwa katika nyumba ya al-Bashir

media Kiongozi wa Baraza la kijeshi, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, alithibitishia maafisa wa polisi, jeshi kwamba kuligunduliwa euro milioni saba, Dola laki 3 na 50,000 na pesa bilioni tano za Sudan. Kwa ujumla, ni zaidi ya euro milioni 100. ASHRAF SHAZLY / AFP

Wakati waandamanaji wakiendelea kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum tangu Aprili 6, kiongozi wa Baraza la mpito la kijeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amefanya mahojiano yake ya kwanza ya televisheni.

Ameelezea nia ya baraza lake la kukabidhi madaraka kwa raia na kuahidi kwamba jeshi bila shaka, litajibu madai ya waandamanaji wiki.

Wakati huo huo Bw Burhan pia ametangaza kwamba wamekamata fedha nyingi katika nyumba ya Omar El Bashir aliyetimuliwa madarakani tarehe 11 Aprili mwaka huu.

Tangu Jumamosi, video imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikionesha mirundo ya manoti ya fedha katika moja ya makaazi ya Omar Hassan al-Bashir.

Siku ya Jumapili, kiongozi wa Baraza la kijeshi, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, alithibitishia maafisa wa polisi, jeshi kwamba kuligunduliwa euro milioni saba, Dola laki 3 na 50,000 na pesa bilioni tano za Sudan ... Kwa ujumla, ni zaidi ya euro milioni 100.

Wakati huo huo waangalizi wamebaini kwamba Mwendesha mashtaka anachunguza madai ya Utakasishaji wa Fedha Haramu dhidi ya Omar al-Bashir.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana