Pata taarifa kuu
JAPANI-G20-USHIRIKIANO-UCHUMI

Tokyo yatoa wito kwa G20 kuimarisha ushirikiano wa kimataifa

Waziri wa Fedha wa Japani Taro Aso ameomba nchi zilizostawi na zinazoinukia kiuchumi za G20, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na vitisho vinavyolenga uchumi wa dunia, katika hali ya mvutano wa kibiashara na ukuaji wa kasi kwa uchumi wa China.

Waziri wa Fedha wa Japani Taro Aso, katika mkutano na waandishi wa habari.
Waziri wa Fedha wa Japani Taro Aso, katika mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Japani, ambayo ni mwenyekiti wa Kundi la G20 mwaka huu, inataka kuimarisha majadiliano juu ya usawa wa uchumi wa kimataifa, kwa matumaini ya kuondokana na nia ya Marekani kwa upungufu wake wa kibiashara wa nchi mbili ambapo inajaribu kutatua kwa kushinikiza kufikiwa mikataba ya nchi mbili.

Akizungumza baada ya chakula cha jioni na wawakilishi wa wizara na benki kuu za G20 Alhamisi wiki hii, Taro Aso aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliwabainishia wenzake haja ya kuchukuwa hatua "kwa ushirikiano wa kimataifa", ambapo amesema "ushirikiano huo unatakiwa kuimarishwa ili kukabiliana na matatizo mbalimbali tunayokabiliana nayo".

Mwakilishi wa Wizara ya Fedha ya Japani amesema kuwa kundi la G20 ni jukwaa bora la kujadili usawa wa kiuchumi duniani. Hakuna mtu katika mkutano huo aliyepinga hoja iliyotolewa na Tokyo, amesema.

Hata hivyo, hoja hii inakinzana na sera ya ulinzi iliyopitishwa miaka miwili iliyopita na Donald Trump, ambaye anataka kwanza kuweka mbele Marekani.

Kikao cha kwanza cha mazungumzo kati ya Marekani na Japani kinatarajiwa kufunguliwa mwanzoni mwa wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.