Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Hali ya wasiwasi yaendelea nchini Sudan

Polisi nchini Sudan jana Jumapili walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum waliojitokeza kuandamana kuelekea katika ikulu ya rais Omar al-Bashir kushinikiza ajiuzulu.

Maandamano dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Sudan, Kharthoum, Januari 6, 2019.
Maandamano dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Sudan, Kharthoum, Januari 6, 2019. AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu wafuasi wa chama tawala nao wakijiandaa kufanya maandamano makubwa juma hili kuonesha uungaji mkono wao kwa rais Bashir ambaye ameweka ngumu kung’atuka.

Polisi mjini Khartoum imesema kuwa haitaruhusu maandamano yoyote kufanyika wakati huu baadhi ya watu wakidai kuwa polisi imezuia hata mkusanyiko wa watu 10.

Katika maandamano ya hapo jana, wanafunzi wa chuo kikuu cha Khartoum pamoja na waalimu wao wamekamatwa na polisi kwa kile wanachodaiwa kuwa ni kuandaa maandamano kinyume cha sheria.

Tangu kuanza kwa maandamano haya ya kupinga kupanda kwa bei ya mkate na kuondoka madarakani kwa rais Bashir Desemba 19 mwaka jana, mamlaka nchini humo zinasema watu 19 wamepoteza wakiwemo polisi wawili.

Lakini shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema watu zaidi ya 40 wameuawa katika maandamano hayo, huku likinyooshewa kidolea cha lawama utawala wa Omar al-Bashir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.