Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHUMI

Mnangagwa: Nina imani sasa kuwa uchumi wa Zimbabwe utaimarika

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa nchi yake imegundua machimbo ya mafuta Kaskazini mwa nchi hiyo, na kusema kuwa ana imani kuwa uchumi utaimarika hivi karibuni.

Serikali iliyoteuliwa na Emmerson Mnangagwa ina lengo la kufufua uchumi uliodorora kwa mikaa kadhaa.
Serikali iliyoteuliwa na Emmerson Mnangagwa ina lengo la kufufua uchumi uliodorora kwa mikaa kadhaa. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Rais Mnangagwa amesema utambuzi huo ni wa kihistoria ambao katika siku zijazo utabadilisha hali ya uchumi wa taifa hilo.

Ugunduzi huo umefanywa na kampuni ya nishati kutoka nchini Australia, Invictus Energy na uchimbaji wa mafuta unatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2020.

Zimbabwe inaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi tangu, hali ambayo ilianza wakati aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kuwanyng'anya Wazungu mashamba yao na kuyakabidhi baadhi ya raia wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.