Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Mvutano wa kibiashara waendelea kutokota kati ya Marekani na China

media Rais wa Marekani Donald Trumpna mwenzake wa China Xi Jinping (kulia) wakutana kando ya mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi G20 huko Hamburg, Ujerumani, Julai 8, 2017. ©REUTERS/Saul Loeb, Pool/File Photo

Baada ya Marekani kuchukua hatua ya kuongeza ushuru mpya wa asilimia 10 kwa bidhaa kutoka China, hatimaye China imesema italipiza kisasi kwa kutoza ushuru wa dola bilioni sitini kwa bidhaa kutoka Marekani.

Wadadisi wanasema tayari nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa zimeingia sasa katika vita vya kibiashara.

Wizara ya fedha ya China imetangaza kwamba inalipiza kile ilichokiita ajenda ya Marekani ya ya kujipendelea na kutaka kuwa na biashara yenye ushindani usio wa usawa.

Hata hivyo Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa atalipiza kisasi ikiwa maamuzi hayo ya China itawalenga wakulima, wafugaji na wafanyakazi kutoka Maekani.

Rais Trump ameitolea wito China kunya mazungumzo na Marekani kwa wakati inayoutaka.

Wakati huo huo China kupitia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Geng Shuang, imesema mazungumzo kati ya China na Marekani ni njia pekee ya kuondokana na mvutano huo.

Rais  Donald Trump, ametangaza kuwa ushuru huu unaolenga bidhaa zenye thamani ya Dola Bilioni 200, zinazoingizwa nchini Marekani.utaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 24 mwezi huu wa Septemba.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana