Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-UCHUMI

Serikali yavunjwa, waziri mkuu mpya ateuliwa Sudan

Sudan imempata waziri mkuu mpya, baada Rais Omar la Bashir kuvunja Baraza lake la Mawaziri. Hii ni hatua ya kukabiliana na mzozo wa kiuchumi uliokumba nchi yake katika miezi ya hivi karibuni.

Rais wa Sudan Omar la Bashir, ambaye serikali yake imekuwa ikikosolewa kushindwa kudhibiti hali ya uchumi.
Rais wa Sudan Omar la Bashir, ambaye serikali yake imekuwa ikikosolewa kushindwa kudhibiti hali ya uchumi. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ilisababishwa na hatua ya serikali ya kuondoa ruzuku ya chakula

Kushuka kwa Sarafu ya Sudan kumesababisha ugumu katika kununua ngano nje ya nchi na bidhaa nyingine.

Motazz Moussa, ambaye alikuwa Waziri anayeshughulikia masuala ya umeme na umwagiliaji. anashika nafasi ya Bakri Hassan Saleh aliyechaguliwa kuongoza nafasi hiyo mwaka 2017.

Hatua hii imechukuliwa kutokana na hali ya kuuchumi ambayo imekuwa ikiongezeka kutokana na kupanda bei za vitu na vingine kutopatikana.

Idadi ya mawaziri katika serikali mpya itapungua kutoka 31 hadi 21, hatua ambayo inalenga kupunguza matumizi. Hata hivyo Hakuna nafasi nyingine za mawaziri zilizotangazwa.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka chma tawala cha National Congress baadhi ya mawaziri ikiwa ni pamoja na waziri wa Mambo ya Nje, ulinzi na masuala ya Rais wataendelea kushikilia nafasi zao.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Sudan imekumbwa na maandamano kila kukicha baada ya bei ya mkate kupanda maradufu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.