sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Siasa - Uchumi

Angola kuondokana na enzi za dos Santos Jumamosi

media Rais mpya wa Angola Joao Lourenço, pamoja na mkewe, akisalimu umati wa watu wakati akitawazwa huko Luanda, Angola, Septemba 26, 2017. © REUTERS

Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos anatarajia kustaafu moja kwa moja katika ukumbi wa siasa Jumamosi wiki hii na kukabidhi uongozi wa chama tawala kwa mrithi wake Rais wa nchi hiyo Joao Lourenço.

Dos Santos ambaye ni mgonjwa kwa sasa, alianza kutawala Angola mnamo mwaka 1979 na aliomba kuachia ngazi kwa amani, kinyume na wenzake wengi wa Afrika.

Mwaka mmoja uliopita, alikataa kujiongeza muhula mpya katika uchaguzi wa urais na kukubali kukabidhi madaraka kwa waziri wake wa zamani wa ulinzi, Joao Lourenço. Hata hivyo, aliendelea kushikilia uongozi wa chama tawala cha MPLA, nafasi ya kuchukua urais mamlaka ya uongozi wa nchi.

Siku ya Jumamosi, "kipenzi nambari moja", mwenye umri wa miaka 76, pia atakabdhi funguo za chama kwa Joao Lourenço, katika mkutano wa chama.

"Kustaafu kwa dos Santos ni hatua muhimu katika mabadiliko ya kisiasa nchini Angola," amesema mchambuzi Alex Vines kutoka kituo cha tathimini cha Uingereza cha Chatham House.

Ndugu zake wamekua wakidhibiti sekta muhimu za uchumi, kama vile kampuni ya mafuta ya kitaifa iliyomilikiwa na binti yake bilionea Isabel. Na washirika wake wa karibu walikua wakisimamia jeshi na polisi.

Lakini, kwa mshangao mkubwa, mtu ambaye alikua kama mtu wake wa karibu, Joao Lourenço haraka alijitoa aliamua kuondokana na mamlaka ya mtangulizi wake kwa kushambulia kwanza mizizi ya utawala wa dos Santos.

Kwa kukabiliana na mdororo wa uchumi na kupambana na rushwa, rais wa sasa aliamua kumtenga Isabel dos Santos kwenye usimamizi wa kampuni ya Sonangol na kaka yake Jose Filomeno, anayejulikana kama "Zenu", kwa fuko la kitaifa la nchi.Jose Filomeno pia alishtakiwa kwa kosa la ubadhirifu mali ya umma.

Katika miezi michache,ndugu na jamaa wengi kutoka ukoo wa dos Santos wameondolewa kwa makini kutoka kwa wakuu wa taasisi, makampuni ya umma na chama.

Hali hii ilizua mvutano mkubwa. Rais wa zamani mwenyewe alionyesha hasira yake hadharani. "Mabadiliko ni muhimu lakini hayapaswi kuwa kuwa yenye msimamo mkali," alisema dos Santos mnamo mwezi Desemba mwaka uliyopita.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana